1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaCanada

Watu 6,000 wayakimbia makaazi yao kutokana na moto Canada

15 Mei 2024

Mamlaka katika jimbo la Alberta nchini Canada limeagiza wakaazi katika eneo maarufu la kuzalisha mafuta la Fort McMurray kuondoka majumbani mwao kufuatia moto mkali unaoendelea kuwaka.

https://p.dw.com/p/4frGu
Moto wa mwituni ukiteteza nyumba katika eneo la Kelowna Magharibi
Moto wa mwituni ukiteteza nyumba katika eneo la Kelowna MagharibiPicha: Darryl Dyck/The Canadian Press/AP/picture alliance

Takriban wakaazi 6,000 wamepewa muda wa mwisho wa hadi saa mbili kuondoka majumbani mwao kutokana na kitisho cha moto unaoenea kwa kasi.

Moto huo - uliopewa jina la MWF 107 - umeenea hadi hekta 9,602 na sasa unachukuliwa kuwa nje ya udhibiti wa mamlaka.

Siku chache zilizopita, maelfu ya watu katika mkoa wa magharibi wa British Columbia pia walihamishwa kutoka majumba yao baada ya moto mkubwa kuzuka karibu na mji mdogo wa Fort Nelson.

Soma pia: Papa Francis aomba radhi kwa makosa ya Kanisa nchini Canada

Nchi hiyo imeshuhudia matukio mengi ya moto mwaka jana huku wataalamu wakifungamanisha matukio hayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Viwango vya juu vya joto pia vimechochea kuongeza msimu wa moto ambao kwa kawaida huanza mwisho mwa mwezi Aprili hadi Septemba au Oktoba.