Watu 37 wauwawa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu 37 wauwawa Afghanistan

Zaidi ya Waafghanistan 37 wameuwawa kwenye shambulio la bomu lililofanywa na mtu wa kujitoa muhanga maisha. Shambulio hilo liliulenga msafara wa magari ya jeshi la kimataifa nchini humo karibu na mpaka wa Pakistan. Duru za polisi zinasema wanajeshi wawili wa kigeni wameuwawa katika hujuma hiyo. Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amelipua bomu lililokuwa ndani ya motokaa katika soko la Spin Boldak. Gavana wa jimbo amethibitisha kwamba msafara ulioshambuliwa ni wa jeshi la Canada nchini Afghanistan. Shambulio la sasa limefanywa siku moja baada ya watu zaidi ya 100 kuuwawa wakati mshambuliaji wy kujitoa muhanga maisha alipojilipua alipokuwa katika umati wa watu katika mji wa Kandahar hapo jana. Maafisa wa Afghanistan wamewalaumu wanamgambo wa Taliban kwa mlipuko huo lakini kundi hilo lililo na mafungamano na kundi la Al Qaeda, limekanusha madai hayo.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com