1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMisri

Watu 32 wapoteza maisha ajali ya barabarani Misri

28 Oktoba 2023

Watu wasiopungua 32 wamefariki dunia leo baada ya basi la abiria kugonga gari lililokuwa limeegeshwa katika barabara kuu inayounganisha mji mkuu wa Misri, Cairo na ule wa mwambao wa bahari ya Mediterania wa Alexandria.

https://p.dw.com/p/4Y9Sz
Ukiukaji kanuni za barabarani ni chanzo cha ajali nyingi nchini Misri
Ukiukaji kanuni za barabarani ni chanzo cha ajali nyingi nchini Misri Picha: AP

Ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi katika mji wa Nubariya, umbali wa kilometa 160 kaskazini mwa Cairo.  Basi hilo la abiria lilikuwa likielekea kwenye mji huo mkuu. Imeelezwa kwamba  hali ya hewa ya ukungu mzito wakati ajali hiyo ilipotokea.

Magari mengine kadhaa yalishika moto baada ya kuliparamia basi lililopata ajali. Wizara ya afya ya Misri imesema mbali ya vifo vya watu 32 wengine 63 wamejeruhiwa kwenye mkasa huo.

Ajali za barabarani zimekuwa zikikatisha maisha ya maelfu ya watu kila mwaka nchini Misri, taifa lenye rekodi mbaya ya kanuni za usalama barabarani.