1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Watu 25 wafariki kufuatia maporomoko ya theluji Afghanistan

19 Februari 2024

Maporomoko ya theluji yamesababisha vifo vya watu 25 wengine kadhaa wakiwa wamekwama katika jimbo la Nuristan, mashariki mwa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4cYzT
Afghanistan | Mwanamke Afganistan akiwa amesimama akisubiri msaada kutoka UNHCR
Mwanamke nchini Afganistan akiwa amesimama huku theluji ikidondoka wakati akisubiri msaada kutoka UNHCRPicha: SHAH MARAI/AFP via Getty Images

Hayo yameelezwa hii leo na afisa wa jimbo hilo baada ya theluji nyingi kumwagika maeneo mengi nchini humo.
      
Mkuu wa idara ya habari na utamaduni wa jimbo hilo, Jamiullah Hashimi, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba bado theluji inamwagika na juhudi za uokoaji zinaendelea, lakini akatahadharisha kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

Soma pia:  Afghanistan yahimiza mazungumzo na jamii ya kimataifa

Maporomoko hayo ya theluji yalikikumba kijiji cha Nakre katika bonde la Tatin la Nuristan usiku wa kuamkia jana huku majumba yakifukiwa kabisa. Takriban nyumba 20 ziliharibiwa vibaya.