1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Afghanistan yahimiza mazungumzo na jamii ya kimataifa

Bruce Amani
30 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan ametoa wito wa kuwepo mazungumzo yenye tija na jamii ya kimataifa, lakini akapinga haja ya kuteuliwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini mwake.

https://p.dw.com/p/4bolD
Kabul Afghanistan | Amir Khan Muttaqi Waziri wa Mambo ya Nje serilaki ya Taliban
Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi akizungumza katika katika mkutano.Picha: Yegor Aleyev/TASS/dpa/picture alliance

Amir Khan Muttaqi aliyasema hayo katika mkutano mjini Kabul uliowaleta pamoja wajumbe maalum na wawakilishi kutoka nchi 11, zikiwemo China, Urusi, Iran, Pakistan na India.

Ametoa wito wakukuza ushirikiano wa kikakanda kwa ajili ya ushirikiano wenye tija ili kupambana na vitisho vilivyopo na vinavyoweza kujitokeza katika kanda hiyo.

Soma pia:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kuteuliwa kwa mjumbe maalum kwa Afghanistan

Serikali ya Taliban mjini Kabul haijatambuliwa rasmi na serikali yoyote nyingine tangu ilipochukua madaraka mwaka wa 2021, na kuweka tafsiri kali ya sheria za Kiislamu ambazo zimewawekea vikwazo wanawake kushiriki katika karibu kila sekta ya maisha ya umma.