1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfghanistan

Afghanistan: Watu 21 wafariki katika ajali ya barabarani

17 Machi 2024

Watu 21 wamekufa na wengine 38 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani katika mkoa wa Helmand kusini mwa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4dokC
Mripuko wa lori la mafuta mjini Kabul
Kikosi cha zima moto wakiwa kazini baada ya kutokea mripuko wa lori la mafuta mjini KabulPicha: Rahmatullah Alizadah/Xinhua/picture alliance

Ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu ya Herat-Kandahar katika wilaya ya Greshk. Polisi wa eneo hilo wamesema ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria kugongana na pikipiki, na kisha dereva wa basi hilo kupoteza udhibiti wa gari lake na kugonga lori la mafuta na kusababisha moto mkubwa.

Watu 11 wapo katika hali mbaya na wanapatiwa matibabu katika hospitali mkoani humo.

Ajali za barabarani zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara nchini Afghanistan, ambako maelfu ya watu hufariki kila mwaka kutokana na ubovu wa barabara, na matengenezo hafifu pamoja na ukosefu wa umakini katika uendeshaji wa vyombo vya usafiri.