1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 20 wapoteza maisha Afghanistan baada ya boti kuzama

Amina Mjahid
1 Juni 2024

Watu wasiopungua 20 wamekufa baada ya boti waliyokuwapo kuzama wakati wakivuka mto mashariki mwa Afghanistan majira ya asubuhi leo Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4gX0d
Afghanistan
Waafghanistan wanatumia sana usafiri wa boti nje kidogo ya mji wa JalalabadPicha: Rahmat Gul/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa idara ya mawasiliano wa jimbo la Nangarhar kulikotokea mkasa huo amesema boti hiyo ilizama kwenye mto unaokatisha wilaya ya Mohmand Dara na miongoni mwa waliopoteza maisha ni wanawake na watoto.

Amesema chombo hicho kilikuwa kimewabeba watu 25 na 5 pekee ndiyo wamenusurika. 

Hadi sasa miili ya watu 5 ndiyo imeopolewa ikiwemo ya mwanaume na wavulana wawili na msichana mmoja.

Afisa huyo amesema magari ya kubeba wagonjwa yametumwa kwenye eneo hilo. Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.