1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu 12 wauawa katika shambulizi la droni nchini Sudan

Tatu Karema
3 Aprili 2024

Shambulizi la droni limesababisha vifo vya watu 12 na kujeruhiwa kwa wengine 30 katika eneo la Atbara lililoko Kaskazini Mashariki mwa Sudan

https://p.dw.com/p/4eMrb
Kiongozi wa kundi la RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Daglo akiwahutubia wapiganaji hao mnamo Julai 28,2023
Kiongozi wa kundi la RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Daglo ( Katikati)Picha: Rapid Support Forces/AFP

Mkazi aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa njia ya simu, amesema kuwa moto ulizuka jana baada ya shambulio hilo lililotokea wakati wa mlo wa kufungua mfungo wa Ramadhani.

Wapiganaji wa kundi la Baraa na raia walikuwa wanashiriki mlo pamoja

Mkazi mwingine ameliambia shirika hilo la habari la AFP kwamba mlo huo uliokuwa umeandaliwa na wapiganaji wa itikadi kali wa Baraa wanaopigana pamoja na jeshi la nchi hiyo, uliwaleta pamoja raia na wapiganaji hao.

Soma pia:Juhudi hizo za upatanishi nchini Sudan bado zitaongozwa na Saudi Arabia na Marekani

Daktari wa hospitali moja katika eneo hilo la Atbara, amesema majeruhi wa tukio hilo pamoja na miili ya waliouawa, walifikishwa hosptalini humo bila ya kubainisha ikiwa walikuwa wapiganaji ama raia.

Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika katika shambulizi hilo.