1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wauwawa katika shambulio la bomu Pakistan

Amina Mjahid
20 Agosti 2023

Wafanyakazi 11 wameuwawa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya bomu lililotegwa kando ya barabara kuripuka Kaskazini Magharibi mwa pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4VMvX
Pakistan | Anschlag auf Polizeifahrzeug
Picha: Mohammad Aslam/AFP/Getty Images

Maafisa wa polisi wa Pakistan wamesema wafanyakazi hao walikuwa wakirejea nyumbani kutoka kazini wakati gari lao lilipogongwa na kilipuzi hicho. 

Kaimu waziri mkuu wa taifa hilo Anwarul Haq Kakar amesema amesikitishwa na kulaani shambulio hilo aliloliita la kigaidi huku akisema anasimama pamoja na familia zilizoathiriwa na mkasa huo. 

Mkuu wa jeshi la Pakistan auonya utawala wa Taliban dhidi ya kuhifadhi makundi ya kigaidi

Eneo hilo la milima la Kaskazini la Waziristan limekuwa likitumiwa kwa muda mrefu na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda kabla ya kufurushwa huko katika msururu wa mashambulizi dhidi yao. 

Pakistan imekuwa ikishuhudia machafuko mara kwa mara kutoka kwa kundi la Taliban la Pakistan tangu wenzao walipochukua madaraka nchini Afghanistan.