1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto kadhaa watekwa nyara katika jimbo la Katsina, Nigeria

Amina Mjahid
3 Novemba 2022

Watoto kadhaa wametekwa nyara na watu waliojihami kwa silaha katika jimbo la Kaskazini la Katsina nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/4J0Gw
Nigeria einige Schulkinder kehren heim | Katsina
Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Polisi pamoja na wakaazi wa eneo hilo wamesema watekaji nyara wanadai kulipwa fidia ili wawaachilie huru.

Katsina ni jimbo la Rais Muhammadu Buhari na ni miongoni mwa majimbo ya Kaskazini Magharibi na Kati ambako wahalifu waliojihami kwa silaha hutumia pikipiki kuwauwa wakaazi au kuwateka nyara na baadaye kudai fidia.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Gambo Isah amethibitisha tukio hilo lakini hakutoa taarifa zaidi.

Wakaazi wamesema watoto hao walichukuliwa kutoka katika mashamba walikokuwa wakivuna mazao karibu na vijiji vya Mailafiya na Kurmin Doka katika jimbo hilo la Katsina.