1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalam wa kiafya waelekea Congo kukabili Ebola

Yusra Buwayhid
14 Mei 2018

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mashirika ya Umoja wa Mataifa wameanza kutuma wataalamu kutoa huduma za dharura za kuzuia kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

https://p.dw.com/p/2xfJK
Symbolbild Ebola-Ausbruch
Picha: picture-alliance/dpa/EPA/A. Jallanzo

Jamhuri ya Kedomkrasia ya Congo pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa pamoja wameanza kutuma timu za wataalamu wa kutoa huduma ya dharura ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaoshukiwa kuwaathiri zaidi ya watu 30.

Mkurugenzi wa Afrika wa Shirika la Afya Duniani WHO, Matshidiso Moeti, ameliambia jana shirika la habari la Reuters kwamba WHO imepata dozi 4,000 za chanjo ya Ebola ya majaribio zinazotayarishwa kutumwa nchini Congo.

Ni visa viwili tu hadi sasa ambavyo vimethibitishwa kwa vipimo vya maabara. Nchi tisa jirani na Congo zimewekwa katika hali ya tahadhari kubwa, ikihofiwa huenda ugonjwa wa Ebola ukakavuka mpaka na kuenea hasa hadi Jamhuri ya Kongo au Jamhuri ya Afrika ya Kati.