WASHINGTON:Marekani yakiri kushambulia Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 10.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Marekani yakiri kushambulia Somalia

Wizara yaUlinzi ya Marekani imethibitisha kuwa ndege za Marekani zilishambulia maeneo ya kusini mwa Somalia dhidi ya wanachama wa kundi la kikaidi la Al Qaida.

Maafisa wa Serikali ya mpito ya Somalia wamesema kuwa kiasi cha raia 20 wameauawa katika shambulizi hilo la Jumatatu.

Marekani inawashutumu wapiganaji wa muungano wa mahakama za kiislam huko Somalia kwa kuwahifadhi magaidi wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulizi ya balozi za Marekani, nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998 ambapo zaidi ya watu 200 waliuawa.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa wanaamini mmoja kati watuhumiwa watatu wa ugaidi ameuawa kutokana na shambulizi hilo.Hata hivyo hawajui ni nani kati ya hao watatu wanaotafutwa.

Marekani kwa muda mrefu imekuwa ikiamini kuwa Abu Talha al Sudan raia wa Sudan, Fazul Abdullah Mohammed raia wa Comoro na raia wa Kenya Salehe Ali Salehe Nabhan wamejichimbia nchini Somalia.

Umoja wa Mataifa ,Umoja wa Ulaya wamelaani mashambulizi hayo ya Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com