WASHINGTON ;Nchi masikini kufutiwa madeni
26 Septemba 2005Matangazo
Benki ya dunia pamoja na shirika la fedha la kimataifa zimeunga mkono makubalino ya kufuta madeni ya nchi masikini kiasi cha dola bilioni 55.
Makubalino hayo yalifikiwa na nchi tajiri kwenye mkutano wao wa Gleneagles nchini Scotland katika mwezi wa Julai.
Mwenyeketi wa benki ya dunia bwana Paul Wolfowitz amesema sasa mkazo lazima uwekwe katika juhudi za kujenga biashara huru duniani.
Mazungumzo juu ya baishara duniani yamekwama, na juhudi sasa zinafanyika ili kuyanasua kwenye mkutano utakaofanyika mwezi desemba.
Wawakilishi wa Shirika la biashara duniani WTO watakutana Hong Kong kwa ajli hiyo.
.