WASHINGTON : Kabila amtaka Bush aendelee kusaidia Congo | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Kabila amtaka Bush aendelee kusaidia Congo

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amemtaka Rais George W. Bush wa Marekani hapo jana kuendelea kuisaidia nchi hiyo wakati kiongozi huyo akichukuwa hatua ya kuleta utulivu kwenye eneo tete mashariki mwa nchi hiyo.

Bush amekuwa na mazungumzo na Kabila katika Ikulu ya Marekani ambaye wiki iliopita alisema wanajeshi wa Congo wameamuriwa kuwapokonya silaha kwa nguvu askari wafuasi wa Generali muasi Laurent Nkunda katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Bush amewaambia waandishi wa habari kwamba wamekubaliana mkakati kwa serikali kuwa na udhibiti wa nchi nzima na kwamba kunakuwepo na utulivu nchi nzima.

Kabila amesema kuendelea kuungwa mkono na Marekani ni muhimu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com