1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Washambuliaji wawaua watu 15 Sudan Kusini

Lilian Mtono
21 Machi 2024

Watu 15 akiwemo mkuu wa mkoa wamefariki dunia, wakati msafara wao ulipovamiwa kwenye mkoa wa mashariki mwa Sudan Kusini wa Pibor karibu na mpaka na Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4dxog
Sudan Kusini| Mzozo
Sudan Kusini inakabiliwa na mzozo uliozuka tangu mwaka 2013. Mapigano ya jamii hasimu ni jambo linalotokea kila wakati nchini humo.Picha: LUIS TATO/AFP

Waziri wa habari wa mkoa huo Abraham Kelang, alisema kuwa vijana wanaoshukiwa kuwa na silaha kutoka kabila la Anyuak kwenye kaunti ya Pochalla, waliuvamia msafara huo siku ya Jumanne.

Sababu ya shambulio hilo haikufahamika mara moja, lakini Kelang alimshutumu kamishna wa zamani ambaye alitimuliwa kutoka wadhifa wake katika kaunti ya Pochalla kwa kuwachochea vijana wa Anyuak.

Mapigano kati ya makundi hasimu ya kikabila nchini Sudan Kusini huzuka mara kwa mara, mara nyingi yakichochewa na wizi wa ng'ombe na mizozo juu ya maliasili au ulipaji kisasi wa mashambulizi yaliyopita. Jamii nyingi zinazozozana nchini Sudan Kusini zimejihami kwa silaha, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano mwaka 2013.