1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

UN: Sudan inakumbwa na moja ya majanga makubwa ya kibinadamu

21 Machi 2024

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa Sudan inakumbwa na moja kati ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu katika historia ya hivi karibuni baada ya karibu mwaka mmoja wa vita nchini humo.

https://p.dw.com/p/4dxOD
Akina mama wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam, karibu na El Fasher Darfur Kaskazini, Sudan.
Akina mama wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam, karibu na El Fasher Darfur Kaskazini, Sudan.Picha: Mohamed Zakaria/MSF/REUTERS

Umoja wa Mataifa umeikosoa jumuiya ya kimataifa kwa kukosa kuchukua hatua kuzuia janga hilo la kibinadamu.

Mkurugenzi wa oparesheni katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA Eden Wosornu, amesema jumuiya ya kimataifa umelifumbia macho mzozo wa Sudan na kueleza kuwa, Wasudan wanakabiliwa na hali ya "kukata tamaa."

Soma pia: Idadi ya walioathiriwa na ghasia yaongezeka kwa 35% Sudan Kusini 

Marekani ambayo ni mfadhili mkuu wa Sudan jana iliahidi kutoa msaada wa dola milioni 47 kwa ajili ya kuzisaidia Sudan na nchi jirani za Chad na Sudan Kusini.

Mapigano yaliyozuka mwezi Aprili mwaka jana kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, Mohamed Hamdan Daglo, yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na uhaba mkubwa wa chakula.