1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Wanne wafa, 19 hawajulikani waliko katika moto Uhispania

John Juma
23 Februari 2024

Watu wanne wameuawa kwenye mkasa wa moto ulioteketeza jengo la orofa 14 mjini Valencia, mashariki mwa Uhispania.

https://p.dw.com/p/4cn3R
Uhispania | Jengo la moto huko Valencia
Jengo likiwaka moto mjini ValenciaPicha: Alberto Saiz/AP Photo/picture alliance

Hayo yamethibitishwa na naibu mkurugenzi wa huduma za dharura jimbo la Valencia Jorge Suarez Torres

Lakini kuna hofu kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa watu 15 wanaoaminiwa walikuwa kwenye jengo hilo hawajapatikana.

Wataalam wamesema jengo hilo lilijengwa kwa vifaa ambavyo vinashika moto kwa haraka, hali inayoelezea kusambaa kwa kasi kwa moto huo ulioanza jana jioni.

Manusura 14 walifikishwa hospitalini wakiwa na majeraha ya moto ya viwango tofautofauti akiwemo mtoto wa miaka 7.