1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso yawatia mbaroni watu 8 wakiwemo 3 wa Ulaya

8 Oktoba 2025

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imetangaza kuwakamata watu wanane wa shirika la misaada ya kibinadamu, wakiwemo raia watatu wa Ulaya, kwa tuhuma za ujasusi na uhaini.

https://p.dw.com/p/51d4n
Urusi Moscow 2025 | Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traoré alipotembelea Chuo Kikuu cha Mendeleev
Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traore alipotembelea Chuo Kikuu cha Mendeleev cha Teknolojia ya Kemikali cha UrusiPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/ZUMA/picture alliance

Waziri wa Usalama, Mahamadou Sana, amesema waliokamatwa ni wanachama wa shirika la INSO lenye makao yake nchini Uholanzi, linalojihusisha na usalama wa mashirika ya misaada. Miongoni mwao ni raia wa Ufaransa, mwanamke mwenye uraia wa Ufaransa na Senegal, raia wa Jamhuri ya Czech, raia wa Mali, na Waburkina Faso wanne. Wengine ni mkurugenzi wa shirika hilo nchini Burkina Faso na naibu wake. Mkurugenzi huyo alishawahi kukamatwa mwishoni mwa Julai, wakati shirika hilo liliposimamishwa kwa miezi mitatu kwa madai ya kukusanya taarifa nyeti bila kibali. Tangu mapinduzi ya Septemba 2022, utawala wa kijeshi wa Burkina Faso imeachana na  ushirikiano wa karibu na nchi za Magharibi, hasa Ufaransa.