1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinzi 178 wa Ecuador wanashikiliwa na magenge ya kihalifu

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2024

Walinzi 178 na wafanyakazi wa gereza wanashikiliwana magenge ya wauza mihadarati nchini Ecuador, wakati mzozo kati ya vikosi vya usalama na magenge hayo ukifikia kiwango cha juu.

https://p.dw.com/p/4b9OU
Ecuador
Maafisa wa usalama wa Ecuador wakiwa tayari Picha: AFP/Getty Images

Walinzi 178 na wafanyakazi wa gereza wanashikiliwana magenge ya wauza mihadarati nchini Ecuador, wakati mzozo kati ya vikosi vya usalama na magenge hayo ukifikia kiwango cha juu.

Taifa hilo dogo la Amerika ya Kusini limetumbukia katika mgogoro baada ya miaka mingi ya kudhibitiwa na magenge ya kimataifa ya kuuza mihadarati ambayo yanatumia bandari zake kusafirisha kokeini hadi Marekani na Ulaya.

Ghasia za wiki hii zimechochewa na taarifa ya mmoja wa vigogo wa magenge hayo anayejulikana kwa jina la Fito, kutoroka gerezani.

Siku ya Jumatatu, Rais Daniel Noboa alitangaza hali ya hatari na amri ya kutotoka nje usiku, lakini magenge hayo yalijibu kwa kutangaza vita, utekaji nyara polisi, kuanzisha milipuko, na kutishia kunyonga watu.