1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ecuador yatangaza vita na magenge ya madawa ya kulevya

Sylvia Mwehozi
11 Januari 2024

Rais wa Ecuador Daniel Noboa ametangaza vita na magenge ya madawa ya kulevya ambayo yanawashikilia walinzi wa magereza, katikati mwa ongezeko kubwa la ghasia.

https://p.dw.com/p/4b6Lq
Ecuador
Wanajeshi wakilinda nje ya ikulu ya rais kufuatia wimbi la ghasia nchini EcuadorPicha: Karen Toro/REUTERS

Rais wa Ecuador Daniel Noboa ametangaza vita na magenge ya madawa ya kulevya ambayo yanawashikilia walinzi wa magereza, katikati mwa ongezeko kubwa la ghasia.

Tangazo hilo linafuatia kitendo cha watu waliokuwa wamejihami na bunduki kufyatua risasi katika studio za televisheni na milipuko katika miji kadhaa.

Soma hapa: Watu wapatao 10 wauwawa Ecuador

Rais huyo ameeleza jana kwamba nchi hiyo iko vitani na haitorudi nyuma katika mapambano na makundi hayo. Siku ya Jumanne, Rais Noboa alitoa orodha ya magenge 22 na kuyataja kuwa ni mashirika ya kigaidi huku akikadiria kwamba jumla ya wanachama elfu 20,000 wa magenge ya kihalifu wanafanya kazi Ecuador.

Mitaa katika mji mkuu wa Quito na mji wa bandari wa Guayaquil ilikuwa kimya jana kuliko kawaida, huku biashara nyingi na shule zikifungwa.