Wakenya waamua leo, kukubali ama kukataa katiba mpya.
4 Agosti 2010Matangazo
Katiba hiyo mpya ni sehemu ya mpango wa mabadiliko unaonuia kuzuwia kutokea tena vurugu katika uchaguzi mwingine mwaka 2012.
Jana Tume hiyo ya uchaguzi ilieleza kuwa haitarajii kutokea tena vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2007, wakati wa zoezi hilo la leo la upigaji kura.
Ulinzi waimarishwa:Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume huru ya muda ya uchaguzi nchini Kenya, Ahmed Issack Hassan, usalama umeimarishwa katika maeneo yanayohofiwa kuzuka vurugu ambapo maafisa zaidi wa polisi wamesambazwa katika maeneo hayo.
Kura hiyo ya maoni ni ya kwanza kupigwa kitaifa baada ya uchaguzi huo mkuu uliosababisha vurugu na mauaji ya zaidi ya watu 1,300.