1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji tisa waliofukuzwa Marekani wawasili Cameroon

1 Mei 2026

Wahamiaji tisa kutoka nchi nne za Afrika waliofukuzwa kutoka Marekani waliwasili wiki hii nchini Cameroon, hii ikiwa sehemu ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/5D7Tf
Marekani Baltimore 2025 | Uhamisho kwa taifa la tatu
Mkazi wa Marekani mwenye uraia wa Salvador Kilmar Abrego Garcia na mkewe Jennifer Vasquez (kushoto) ) wafikishwa katik afisi ya uhamiaji Baltimore Maryland mnamo Agosti 25, kwa lengo la kumhamisha Garcia hadi Uganda.Picha: Roberto Schmidt/AFP

David amesema wahamiaji hao waliowasili nchini humo siku ya Jumatano ni raia wa Ghana, Angola, Ethiopia na Congo-Brazzaville na walikuwa kundi la tatu la uhamishaji huo tangu Januari.

Wameungana sasa na wahamiaji wengine kumi na saba waliofukuzwa awali na Marekani hadi Cameroon.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, Marekani inailipa Cameroon dola milioni 30 kuwa sehemu ya mpango huo.

Nchi nyingine za Afrika zilizofikia makubaliano kama hayo ni Equatorial Guinea, Ghana, Rwanda, Sudan Kusini, Eswatini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.