Wageni rukhsa sasa kuingia Mynmar | Masuala ya Jamii | DW | 23.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Wageni rukhsa sasa kuingia Mynmar

Lakini mashirika ya misaada yanataka ufafanuzi zaidi

default

Wakazi wa Ragoon wakikata miti ilioangukia nyaya za umeme pamoja na kuharibu nyumba kutokana na kimbunga Nargis. Wiki tatu baada ya kimbunga hicho kutokea sasa utawala wa kijeshi unakubalia wafanyakazi za kimisaada wa kigeni kuingia nchini humo.

Viongozi wa kijeshi wa Mynamar wanasemekana kukubali wafanyanyakazi wa kimisaada kutoka nje kuingia nchini humo kwa shughuli za misaada.

Hata hivyo tangazo hilo limepokelewa kwa uangalifu na makundi ya utoaji msaada ya kimataifa,yakisema baado maelezo zaidi hayajatolewa.

Makundi ya utoaji msaada,mbali na kufurahishwa na habari njema kufuatia mazungumzo kati ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon na kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, Than Shwe,yanasema kuwa juhudi za utoaji msaada zinahitaji mengi zaidi mbali na kukubaliwa kwa wageni kwenda katika mji mkuu wa Yangoon.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duaniani WFP Paul Risley akiwa katika nchi jirani ya Thailand,amesema kuwa suala muhimu ambalo halijatatuliwa ni ikiwa watakubaliwa kuondoka mji mkuu na kwenda sehemu za mashambani au laa.

Generali Than Shwe ametoa ruhsa wa kuingia kwa wageni baada ya mkutano wake wa saa mbili na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ujumaa asubuhi kwa saa za Mynmar.

Lakini John Sparrow wa shirikisho la kimataifa la vyama vya msalaba mwekundu pamoja na mwezi mwekundu,anasema kuwa tangazo hilo kidogo haileweki na linahitaji ufafanuzi zaidi. Ameendelea kusema kuwa ruksa huu haufafanui nani anakubaliwa kuingia na wapi anapaswa kwenda.

Mashirika ya utoaji msaada yamesema kuwa wataalamu wa kigeni wanahitajika sana ili kutathmini shughuli nzito za kusimamia na kutathmini msaada wa janga.

Hadi sasa kazi hiyo ilikuwa inafanywa na wafanya kazi wa ndani tu ambao wamekubaliwa kuingia katika maeneo yaliyoathirika na kimbunga cha Nargis.

Utawala wa kijeshi umekuwa haukubali wageni kutembelea eneo la kusini la Irrawady ambalo liliathirika vibaya na kimbunga hicho wakati kilipovuma Mai 2 hadi mai 3.

Msemaji wa shirika la World Vision,James East, moja wa mashirika mengi ya kigeni yaliyokataliwa kuendesha shughuli za misaada na utawala wa kijeshi, ana sema kuwa wanasubiri kuona maana kamili ya hali ya tangazo hilo.Ameongeza kuwa mada ya mijadala ya wiki kadhaa zilizopita ilikuwa siasa, na kuongeza kuwa hilo limepita na ni wakati sasa wa kuwasaidia waathiriwa.

Nae waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,Bi Condoleeza Rice,katika mahojiano na shirika la utanagazaji la Uingereza aligusia suala la siasa akisema kuwa mara hii sio siasa bali kusaidia wananchi.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu takriban laki moja thelathini na tatu elf wakiwa wamepoteza maisha yao ama hawajulikani walipo na wengine zaidi ya milioni 2 unusu wakihitaji msaada wa dharura.

Baada ya wiki tatu kupita tangu janga hilo kutokea misaada ya kimataifa imeweza tu kufikia asili mia 25 ya waliothirika.

 • Tarehe 23.05.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E4pD
 • Tarehe 23.05.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E4pD
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com