1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafugaji Kenya wataka kiangazi kutangwa janga la taifa

Shisia Wasilwa
22 Septemba 2022

Wabunge kutoka jamii za wafugaji nchini Kenya sasa wanaitaka serikali kutangaza kiangazi kuwa janga la taifa. Aidha wanaitaka serikali kufungua mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori kwa malisho ya mifugo wao

https://p.dw.com/p/4HD88
Kenia Dürre an der Grenze zu Äthiopien
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Kikundi cha wabunge hao kinasema kuwa hali ya kiangazi katika majimbo yao ni mbaya mno na inahitaji kuangaziwa kwa dharura. Kundi hilo lenye zaidi ya wabunge 100 kutoka majimbo 15. Yumkini watu milioni 4.1 kutoka majimbo hayo wanakabiliwa na baa la njaa. Wakiongozwa na mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale na Mwenyekiti wao Bashir Abdullah wa Mandera Kaskazini, wameihimiza serikali kutenga fedha nyingi zaidi ili kuwasaidia wakazi wa majimbo yao. "Tunahitaji mikakati ya dharura, mifugo wanakufa kwa kukosa maji, na kuchimba visima vingine kwa sababu ya idadi kubwa ya mifugo na watu wanaohitaji maji."

Tamko lao linajiri baada ya rais aliyeondoka Uhuru Kenyatta kutangaza hali hiyo kuwa janga la taifa mwezi septemba mwaka uliopita. Tangazo hilo lilifungua milango ya misaada katika majimbo yaliyokuwa yameathiriwa.  Maelfu ya mifugo wameangamia kwa uhaba wa maji na lishe. Wabunge hao sasa wanasema kuwa kutokana na mzozo wa lishe miongoni mwa jami za wafugaji, kuna hatari ya makabiliano katika ya wafugaji. Mohamed Adow ni mbunge wa Wajir.

Duale ameihimiza serikali kuhakikisha kuwa chakula na msaada wa kutosha vimesambazwa katika majimbo yanayojitaji chakula kwa dharura. Aidha wabunge hao wameiomba serikali kuharakisha mpango wa kuwapa wazee fedha pamoja na kuchimba visima vya maji.  Shadrack Kalasa ni afisa wa msalaba mwekundu.

Duale amezitaka jamii za wafugaji kushirikiana badala ya kuzozania maji na lishe inayopatikana kwa uhaba. Shirika la msalaba Mwekundu linasema kuwa watu 378,000 katika kaunti ya Garissa wanakabiliwa na baa a njaa na idadi hiyo inaongezeka kila kukicha.