Wafanyakazi wahamiaji | Masuala ya Jamii | DW | 17.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Wafanyakazi wahamiaji

Uhamiaji-faida na athari zake kwa nchi changa.

Zaidi ya watu milioni 200 kutoka kila pembe ya dunia, wanaishi na kufanya kazi nchi za nje na wengi wao, ni wafanyikazi waliohamia nchi hizo.Katika hali hii ni taabu kupima kati ya mambo mawili: kupoteza utaalamu kwa nchi zao (Brain Drain) na kunufaika nchi hizo kwa fedha za kigeni wanazopeleka nyumbani.

Umasikini,njaa,misiba ya kimaumbile au mapigano nchini mwao, mara nyingi huwa sababu kwanini wanadamu wanazihama nchi zao za asili na kutafuta kazi nchi za kigeni.Hata tofauti ya mishahara iliopo baina ya nchi na nchi duniani ni sababu nyengine zinazowavutia wafanyikazi kuhama nchi zao na kuhamia kwengine kwenye mishahara bora.

Imeonekana hasa kuhama kwa watu kutoka nchi changa kwenda nchi zilizoendelea kumekuwa hatua kwa hatua kukiongezeka.

3% ya wakaazi wa sayari hii-kwa muujibu wa makisio ya Shirika la kimataifa la uhamiaji -International Organisation for Immigration (IOM),wanaishi wakati huu kama wageni waliohamia nchi za nje na nusu yao ni wanawake.

mmojawao ni Mera Gocotano:

"Miaka 3 nikifanya kazi katika shule hii na awali niliridhika.Baadae lakini, gharama za chakula,umeme na ada za shule za dada yangu zliongezeka mno.mara kila kitu kikawa ghali ."

Mera Gocotano au kutoka Davao,kisiwa cha kusini kabisa cha Mindano huko Philipine akiwa mwalimu nchini mwake hapati mshahara unaopindukia kiasi cha Euro 80 kwa mwezi.Mjini Hongkong, ambako sasa anatumika katika nyumba ya ukoo tajiri,analipwa mshahara mara 5 mkubwa zaidi kuliko ule aliopata nyumbani Mindano.

Ili kupatiwa kazi hiyo nchi ya nje na ada zote za hati ilimgharimu Euro 1.200.

Kuhamia nchi ya nje ni biashara kubwa .Nyumbani anafaidika aliekupatia kibarua hicho kwa kazi yake ya kukuhudumia kukupatia ruhusa ya kufanya kazi,visa,pasi ya kusafiria na kazi yenyewe.

Huko ngambo,halkadhalika, yamatia fedha pia mashirika yanayotoa huduma za maskani ya kuishi na mawsasiliano na bila shaka hata makampuni ambayo ama yanatoa wafanyikazi wanaolipwsa ujira mdogo au wanaolipwa ujira nafuu kwa makampuni au hata wataalamu wenyewe ujuzi maalumu kutoka ngambo kwavile nchini hakuna wsa kutosha.

Vitita vya fedha ambavyo wafanyikazi hawa waliohamia nchi hizi wanazotuma makwsao nchi changa au zinazoinukia kiuchumi,ni viwango vikubwa kwa jicho la uchumi wa dunia.

"Fedha zinazopelekwa nyumbani kutoka nje zinafikia kima cha dala bilioni 300 kwa mwaka na hiki ni kingi mara 3 kuliko msaada mzima wa maendeleo unaotolewa."

Anasema Robert Calderisi,meneja wa zamani wa Banki kuu ya Dunia barani afrika na mtungaji wa kitabu "The Trouble with Afrika Why foreign Aid isnźt working"-"shida na bara la Afrika-kwanini misaada kutoka nje haifanyi kazi."

Anasema sehemu kubwa ya fedha hizo,kwa makadirio ya karibuni ya shirika la kimataifa juu ya uhamiaji (IOM) humiminwsa katika zile nchi changa ambazo katika msukosuko wa sasa wa fedha ulimwenguni,zinahitaji mno fedha hizo.

Kwa nchi kama Philippines fedha zinazoletwas nchini na wahamiaji wake nchi za ngambo ndio chemchem kubwa ya mapato yake ya fedha za kigeni.Kiasi cha wsaphilipino milioni 10 wanatumika nchi za nje wakati nyumbani kwa mfano,kuna ukosefu wa walimu ,madaktari na wauguzi .60% ya wakaazi wake wanaishi katika hali za ufukara.Hali ya mambo kama hii haifahamiki: Kwani, wafanyikazi wenye ujuzi maalumu unaotakikana nchini,wanatumika nchi za nje kama mabingwa kwavile nyumbani hawapati kazi za kuwaridhisha.

Mfano mwengine ni afrika Kusini: Kwa muujibu wa taarifa zake binafsi,Afrika kusini ilitia raslimali kuanzia 1994 hadi 2000 ya kiasi cha dala bilioni 1 kunyanyua elilumu ya watumishi wake wa matibabu na afya ambao baadae walihamia nchi nyengine zinazozungumza kingereza mfano wa uingereza na Marekani.Afrika kusini yenyewe ili kukidhi mahitaji yake inaajiri wafanyikazi kama madaktari,wauguzi wa mahospitali kutoka nchi jirani kama Malawi.Na Malawi kwenyewe ,mojawapo ya nchi masikini duniani,kiasi cha thuluthi-mbili ya nafasi za kazi upande huo hazina mtu.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com