Wacameroon watoweka katika michezo ya Jumuiya ya Madola | Matukio ya Afrika | DW | 11.04.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Wacameroon watoweka katika michezo ya Jumuiya ya Madola

Maafisa wa timu ya Cameroon inayoshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea Australia wamesema wanamichezo watano kutoka kambi yao wametoweka.

Wanyanyua vyuma watatu na mabondia wawili hawajaonekana tangu jana na kuzua tetesi kwamba wametoroka wakiwa na nia ya kutorudi Cameroon. Tukio hilo limeripotiwa kwa polisi wa Australia.

Afisa wa Cameroon aliyezungumza na vyombo vya habari, Simon Molombe, amesema ameshtushwa alipofahamu kwamba wanyanyuwa vyuma, Oliver Matam Matam Arcangeline Fouodji na Petit Minkoumba, pamoja na mabondia - Christian Ndzie Tsoya na Simplice Fotsala - wametoweka.

Waandalizi wa michezo ya Jumuiya ya Madola wamewataka washiriki waheshimu sheria, ikizingatiwa kwamba zaidi ya wanariadha 100 walipitisha muda wa kurudi katika visa zao katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2000 huko Sydney.