1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji waharibu viwanda, mashamba Ethiopia

Sylvia Mwehozi
7 Oktoba 2016

Vyombo vya habari vinaripoti kuharibiwa viwanda 11, mashamba kadhaa ya maua na zaidi ya magari 60 katika machafuko ya hivi karibuni kabisa nchini Ethiopia kufanywa na waandamanaji wanaoipinga serikali.

https://p.dw.com/p/2R0Kg
Äthiopien Tote bei Anti-Regierungs-Protesten in Bishoftu
Picha: DW/Y. Gegziabher

Kituo cha matangazo cha FANA; ambacho kinaonekana kuwa karibu na serikali, kimeripoti kupitia tovuti yake kwamba makampuni yaliyoathirika yalikuwa yametengeneza ajira 40,000 katika taifa hilo; wakati uzalishaji wa viwanda ukiathiriwa zaidi na machafuko katika jimbo la Oramiya.

Orodha ya viwanda vilivyoharibiwa ni pamoja na kiwanda cha nguo cha Kituruki cha Saygin Dima, ambapo meneja wake anasema robo tatu ya mimea imeharibiwa kwa moto.

Radio hiyo imesema mashamba mengine mawili ya maua, kiwanda kingine cha nguo na kiwanda cha kutengeneza plastiki pia vimeharibiwa.