1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Vyama nchini Pakistan vyakubaliana kuunda serikali ya mseto

Zainab Aziz
14 Februari 2024

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif, amesema chama chake kitaunda serikali ya mseto pamoja na chama kingine kikubwa na vingine vidogo ili kuumaliza mkwamo uliotukia baada ya kufanyika uchaguzi nchini Pakistan.

https://p.dw.com/p/4cO5F
Lahore, Pakistan | Waziri Mkuu wa zamani Nawaz Sharif
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz SharifPicha: K.M. Chaudary/AP/picture alliance

Chama cha waziri mkuu huyo wa zamani, Muslim League PML-N kitaunda serikali kwa kushirikiana na chama cha PPP cha Bilawal Bhutto Zardari, kuunda serikali, pamoja na vyama vingine.  

Kwa pamoja vitakuwa na viti vya kutosha bungeni. Hapo awali vyama vya PML-N na PPP vilikuwamo katika mseto uliomwondoa madarakani waziri mkuu Imran Khan mnamo mwaka 2020.

Soma pia:Vyama vya Pakistan vimekubaliana kuhusu muungano

Hata hivyo wagombea huru, waliokiwakilisha chama cha Imran Khan PTI ndio waliopata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huo. Nawaz Sharif anapanga kumteua mdogo wake Shehbaz Sharif, kuwa waziri mkuu.