Vurugu zazuka Albania | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Vurugu zazuka Albania

Polisi wajaribu kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali ya waziri mkuu Sali Berisha. Waandamanaji hao wanataka serikali ijiuzulu kutokana na madai ya rushwa.

default

Magari kadhaa ya polisi yaliwashwa moto katika vurugu hizo

Watu watatu walipigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Albania Tirana hapo jana, wakati waandamanaji walipokabiliana na polisi katika mkutano wa upinzani dhidi ya serikali.

Albanien Ministerpräsident Sali Berisha

Waziri mkuu Sali Berisha.

Waziri mkuu Sali Berisha amewataja waandamanaji hao kuwa jaribio la upinzani kuanza machafuko yalio mfano wa Tunisia. Chama cha upinzani cha kisoshalisti kimekataa kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2009 ambapo chama cha waziri mkuu Berisha kilishinda kwa tafauti ya kura chache tu. Vurugu hizo zilizuka wakati waandamanji walipokusanyika nje ya ofisi ya waziri huyo mkuu,wakiitaka serikali yake ya kihafidhina ijiuzulu kutokana na madai ya rushwa. Magari kadhaa ya polisi yaliwashwa moto na waandamanaji waliwarushia polisi mawe na vigongo, wakilishambulia pia jengo hilo.

Tirana Albanien Protest

Polisi walijibu kwa kutumia hewa ya kutoa machozi, mipira ya maji, na risasi za mpira kujaribu kuwatawanya waandamanaji hao.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Afp/Rtre
Mhariri: Abdul-Rahman.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com