1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zaendelea kushuhudiwa nchini Tanzania

31 Oktoba 2025

Huduma za intaneti zimekatizwa kwa siku ya tatu leo nchini Tanzania huku ripoti za maandamano zaidi ya kupinga uchaguzi zikiibuka na upinzani kukataa matokeo ya uchaguzi katika kisiwa cha Zanzibar.

https://p.dw.com/p/52sMC
Tansania Arusha 2025 | maandamano ya uchaguzi
Maandamano ya ghasia mjini Arusha TanzaniaPicha: AP Photo/picture alliance

Kutokana na mashirika ya habari ya kigeni kupigwa marufuku kwa kiasi kikubwa kuripoti uchaguzi huo na kizuizi cha mawasiliano kuingia siku yake ya tatu, upatikanaji wa taarifa za kutosha umekuwa mgumu.

Mashuhuda katika mitaa ya Sinza mjini Dar es Salaam na kwenye mji mkuu Dodoma, wameliaambia shirika la habari la AFP kwamba maandamano yaliyozuka siku ya Jumatano yameendelea hadi jana usiku huku watu wakichoma matairi.

Watu kadhaa wahofiwa kuuawa katika ghasia Tanzania

Kumekuwa na ripoti za idadi kubwa ya vifo lakini bado haijathibitishwa na hospitali nyingi na kliniki za afya zimekataa kutoa taarifa.

Taarifa pekee rasmi ilitolewa jana jioni na Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo Jenerali Jacob Mkunda ambaye amewaita waandamanaji hao "wahalifu".

Jenerali Mkunda, amelaani vurugu hizo na kusema jeshi hilo litashirikiana na taasisi nyingine za usalama kudhibiti hali hiyo.