1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Vitendo vya utekaji nyara vinazidi kuongezeka Sahel

Angela Mdungu
10 Novemba 2023

Makundi yenye itikadi kali za Kiislamu yamekuwa yakitishia maeneo mengi ya Sahel. Serikali huko zimeangushwa na kwa mapinduzi ya kijeshi yanayopambana na makundi ya kigaidi kwa kushirikiana na vikosi Wagner.

https://p.dw.com/p/4Yfme
Raia wa Burkinafaso wanaopitia madhila mengi katika ukanda wa Sahel
Raia wa Burkinafaso wanaopitia madhila mengi katika ukanda wa SahelPicha: MSF/Nisma Leboul

Kulingana na utafiti wa taasisi ya masomo ya usalama, watu 180 walitekwa nyara Mali na Burkina Faso katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Mmoja wa watu waliowahi kunusurika na vitendo vya aina hiyo ni kijana Patrick ambaye hakutaka jina lake halisi litajwe. Yeye ni muuguzi katika kliniki binafsi.

Anakumbuka  vyema kilichotokea Juni 15.  Alikuwa amekaa kwenye basi katika Barabara kuu katikati mwa Mali. Basi lilisimama.  Ni wanamgambo wenye itikadi kali waliomlazimisha dereva kulisimamisha.

Patrick alishikiliwa na magaidi kwa miezi miwili. Wakati huo aliwahudumia mateka wengine na waliokuwa na matatizo ya afya. Alilazimika kujifunza Koran na hata kuswali na watekaji. Alipokataa, alipigwa. Wengine walifanyiwa vibaya zaidi.

Mali, Niger, Burkina Faso wanakabiliwa na uasi wa jihadi kwa muda mrefu

Agosi 15, siku mbili kabla ya kutimia miezi miwili ya kutekwa kwake wanamgambo hao wenye itikadi kali walimuachilia huru. Baadaye, Patrick aligundua kuwa aliachiliwa huru kutokana na makubaliano ya kubadilishana wafungwa ambapo wanamgambo wengine wa itikadi kali waliokuwa wakishikiliwa waliachiliwa.

Mtaalamu wa sayansi ya siasa raia wa Ufaransa Flore Berger anayefanya kazi katika taasisi inayofuatilia uhalifu wa kupangwa ya mjini Geneva anasema watu wanaposoma au kusikia kuhusu utekaji nyara kupitia vyombo vya habari vya magharibi mara nyingi ni kuhusu wale wanaoachiliwa baada ya kulipa fedha za kuwakomboa zenye thamani ya mamilioni. Hata hivyo hakuna anayezungumzia idadi jumla ya watu wa Sahel ambao wengi wao ndiyo wanaoathirika.

Wastani wa mtu mmoja hukamatwa kila siku Mali na Burkina Faso 

Baadhi ya Makundi ya wanamgambo katika Ukanda wa Sahel
Baadhi ya Makundi ya wanamgambo katika Ukanda wa SahelPicha: Inside the Resistance

Hivi karibuni, Berger aichapisha utafiti unaoonesha kuwa wastani wa mtu mmoja hukamatwa kila siku Mali na Burkina Faso kwa mwaka huu. Ingawa waasi na vkosi vya kulinda usalama nao wanawateka watu nyara pia, visa vingi ni kazi ya magaidi wenye itikadi kali. Vinara wa utekaji  kwenye ukanda huo ni kundi la  Jamāʿat Nusrat al-Islām wa-l-Muslimīn. Berger anasema, kwa makundi hayo, kufanya hivyo ni njia muhimu ya kutoa vitisho.

Ujerumani na Ulaya kusaidia kuimarisha usalama Afrika Magharibi

Pamoja na hayo, mikakati ya makundi hayo ya itikadi kali hubadilika. Kama madhumuni yao ni kujinyakulia eneo fulani, utekaji nyara hutumika kuwaadhibu watu ambao hawatii. Hatua inayofuata ni kuonesha udhibiti wao katika eneo fulani.  Kulingana na mtaalamu wa sayansi ya siasa Flore Berger, wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa ya misaada kwa mfano, hukamatwa na kushikiliwa kwa saa 24.  Hata hivyo anasema wakati mwingine ni vigumu kwani ikiwa magaidi wakihisi kuwa mateka wanayemshikilia anafanya kazi katika mamlaka za nchi au jeshini basi mtu huyo anaweza kuuwawa mara moja.

Na hiyo ndivyo ilivyotokea kwa rafiki wa karibu wa kijana Ousmane Guindo. Siku moja walikuwa wakisafiri pamoja katika mji wa Timbuktu nchini Mali. Walisimamishwa na wanamgambo wenye itikadi kali. Waliamriwa kufungua mabegi yao na kuwapa simu. Hawakuona kitu chenye maslahi kwao isipokuwa waliona picha ya rafiki huyo akiwa na sare za jeshi katika simu ya mkononi ingawa hakuwa mwanajeshi. Walimchukua na hadi sasa hajulikani aliko. Gindo na familia ya rafikiye wana uhakika aliuwawa na hicho si kisa pekee katika ukanda wa Sahel