1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mali, Niger na Burkina Faso kuashirikiana kupambana na uasi

Lilian Mtono
17 Septemba 2023

Mali, Niger na Burkina Faso zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama, wakati mataifa hayo yakipambana na uasi ulioanzia kaskazini mwa Mali mnamo mwaka 2012 na kusambaa hadu Niger na Burkina Faso mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/4WRT0
Kiongozi wa kijeshi nchini Mali Assimi Goita amesema wanalenga kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel
Kiongozi wa kijeshi nchini Mali Assimi Goita amesema wanalenga kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi katika eneo la SahelPicha: Habib Kouyate/Xinhua/IMAGO

Kiongozi wa kijeshi wa Mali Assimi Goita amesema kwenye mtandao wa X kwamba amesaini makubaliano na mataifa hayo, yanayoitwa Liptako-Gourma yenye lengo la kuanzisha mkakati wa pamoja wa kuisalama.

Eneo la Liptako-Gourma ambako mipaka ya Mali, Burkina Faso na Niger inakutana limekuwa likikabiliwa na uasi wa jihadi kwa miaka mingi sasa.

Kulingana na waziri wa ulinzi wa Mali Abdoulaye Diop, mataifa hayo matatu ambayo yamepitia mapinduzi ya kijeshi tangu mwaka 2020, yatashirikiana kijeshi na kiuchumi na kipaumbele chao kitakuwa ni kupambana na ugaidi.