1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita dhidi ya ugaidi na kumbukumbu ya Septemba 11

11 Septemba 2021

Miaka 20 iliyopita, magaidi waliitikisa Marekani, taifa lenye nguvu duniani. Taifa hilo lilitangaza vita dhidi ya ugaidi. Dunia itapaswa kuendelea kupambana na matokeo ya vita hiyo anasema Matthias von Hein wa DW.

https://p.dw.com/p/40AO6
USA | New York Ground Zero
Picha: Hundt/Eibner/imago images

Sasa, minara ya kituo kipya cha biashara, World trade Center, imesimama mjini New York, ikiwa na kumbukumbu ya takribani watu 3,000 walioathiriwa na shambulio hilo lililoishtua Marekani na dunia kwa ujumla. 

Miaka mingi imepita tangu mashambulizi ya Septemba 11.  Si tu Marekani inayoandaa kumbukumbu ya siku hii bali pia maeneo mengine ya mashariki ya kati na hata Afghanistan. 

Huko, bendera ya Taliban inapepea tena, kama ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Hivi karibuni kulipotokea shambulio la kigaidi lililowaua raia 170 wa Afghanistan na wanajeshi zaidi ya kumi wa Marekani wakati wa operesheni ya kuwaondoa watu katika uwanja wa ndege wa Kabul, kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS lilitangaza kuwa lilihusika na shambulio hilo.

Kundi hili wala halikuwepo miaka 20 iliyopita wakati vita dhidi ya ugaidi vilipoanza. Hata hivyo asili yao ina uhusiano na vita hivi na namna vilivyopiganwa kama anavyoeleza mwanahistoria kutoka Hamburg Bernad Greiner

USA | Terroranschlag am 11. September 2001
Picha ya shambulio la ugaidi la Septemba 11Picha: Chao Soi Cheong/AP/picture alliance

''Tunafahamu fika kwamba kukua kwa kundi linalojiita dola la kiislamu IS kulikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya kuangushwa kwa utawala wa Saddam Hussein. Sehemu kubwa ya kizazi cha kwanza cha wapiganaji wa ISIS kilitokana na jeshi la zamani la Saddam Hussein ambalo Marekani imelisambaratisha mamia kwa maelfu ya vijana wadogo walikuwa mitaani bila matumaini ya kuwa na ajira. ''

Mwaka 2001, kundi la kigaidi la al-Qaeda liliishambulia jengo la World Trade center ambalo ni alama ya uwezo wa kiuchumi. Walishambulia jengo la wizara ya ulinzi, Pentagon ambalo ni kituo cha nguvu ya kijeshi.  Magaidi hao hawakutumia kitu kingine zaidi ya visu vya kukatia maboksi walivyokuwa navyo wakaigeuza ndege ya abiria kuwa silaha wakiongozwa na raia wa Saudia, Osama bin laden akiwa ndani ya hema huko Aghanistan.

USA | Terroranschlag am 11. September 2001
Picha: picture-alliance/ dpa

Marekani ilihuzunishwa na kufadhaishwa na dunia nzima ilisimama nayo. Ilitawala kwa hasira ikitafuta kulipa kisasi. Operesheni iliyohusisha vikosi maalumu miaka kumi baadaye katika kumuuwa kiongozi wa  al-Qaeda Osama bin Laden, akiwa Pakistan haikuwa suala la mjadala kwa utawala wa Marekani. Katika hatua ya kijeshi iliyohalalishwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kama hatua ya kujilinda, utawala wa Taliban ulipinduliwa Afghanistan ndani ya miezi michache.

Wakati Rais wa wakati huo wa Marekani George  Bush alipoishambulia Iraq mwaka 2003, hakukuwa tena na uhalali wa kufanya hivyo. Kulikuwa na madai ya uongo pekee kuwa Saddam Hussein alihusika na washambuliaji wa Septemba 11, pamoja na madai ya uwongo kwamba Rais huyo wa Iraq alikuwa akizalisha silaha za maangamizi.

Vita dhidi ya ugaidi iliyotangazwa na Bush iligeuka kuwa isiyo na mipaka. Mwanahistoria wa Marekani Stephen Wertheim anasema, wanasiasa wa Marekani walitaka kuonesha nafasi ya taifa hilo duniani:

"Nadhani baada ya Septemba 11, viongozi wengi wa Marekani waliona nafasi ya kuonesha kuwa Marekani ni taifa muhimu duniani, na kwahakika lingeonesha umuhimu wake kwa kujaribu kuunda upya nchi zote na maeneo yote ya dunia". 

Kwa mujibu wa  "Gharama ya vita", miaka 20 ya  "vita dhidi ya ugaidi", gharama kwa Marekani pekee ni takribani dola trillioni nane. Fedha hizo zingeweza bila shida kugharamia mara kadhaa programu ya miundombinu ya Rais wa sasa Joe Biden. Na ndio maana mtaalamu Bern Greiner wa Marekani anahitimisha kwa kusema bila kujali matokeo kwa dunia nzima, Marekani imepata hasara kubwa kutokana na gharama za kutisha za vita kwenye mataifa ya Iraq na Afghanistan.