1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Libya wakubaliana kuunda serikali mpya ya umoja

11 Machi 2024

Viongozi watatu wakuu wa Libya wametangaza makubaliano juu ya "umuhimu" wa kuunda serikali mpya ya umoja ambayo itasimamia uchaguzi uliochelewesha kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4dMr4
Libya Tripoli 2023 | Mkutano kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Rais wa Libya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria
Mkutano kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Rais wa Libya,Mohamed al-Menf na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Ramtane LamamraPicha: Libyan Prime Ministry Press Office/Anadolu Agency/picture alliance

Viongozi hao ni rais wa Baraza la Rais (PC) Mohamed Menfi, mkuu wa Baraza Kuu la Serikali (HSC) Mohamed Takala, ambao wote wanaishi Tripoli, na Aguila Saleh, spika wa Baraza la Wawakilishi (HoR) la huko mjini Benghazi.

Katika taarifa ya pamoja, viongozi hao watatu pia wametoa wito kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na jumuiya ya kimataifa kusaidia ufanikishwaji wa mapendekezo yao.

Mchakato wa kisiasa wa kutatua mzozo  wa zaidi ya muongo mmoja nchini Libya ulikwama tangu kuporomoka kwa uchaguzi  Desemba 2021 huku kukiwa na mizozo kuhusu uhalali wa wagombea wakuu.