1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa China wasusia mkutano wa ulinzi Singapore

29 Mei 2026

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth, anatarajiwa kuhutubia katika mkutano wa kilele wa ulinzi wa mataifa ya bara Asia wa Shangri-La Dialogue unaofunguliwa leo huko Singapore.

https://p.dw.com/p/5EX3x
IISS Shangri-La Dialogue 2026 | US-Pete Hegseth
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth Picha: Edgar Su/REUTERS

Maafisa wakuu wa China hawatakuwepo katika mkutano huo wa siku tatu, ambao utajadili masuala muhimu kama mgogoro wa Taiwan na Beijing pamoja na vita vya Iran.

Hii ni mara ya pili kwa Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun, kutoshiriki mkutano huo unaowaleta pamoja maafisa wa ulinzi kutoka mataifa 45. Hii inamaanisha Jun hatokuwa na mkutano na Hegseth wakati ambapo China imetoa onyo kali kwa Marekani kwamba iwe makini kwa namna inavyoishughulikia Taiwan.

Hivi karibuni Rais Donald Trump alifanya ziara ya siku mbili Chini akitaka nchi hiyo iisaidie kuishinikiza Iran kufungua njia ya bahari ya Hormuz. 

China inazingatia kisiwa cha Taiwan kinachojitawala chenyewe kuwa sehemu ya eneo lake.