1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi mafisadi washtakiwa Kenya

3 Julai 2018

Kwa mara ya kwanza Kenya inajitayarisha kumshtaki gavana wa kaunti pamoja na maafisa wengine tisa katika kesi inayohusiana na rushwa. Ni hatua inayoonyesha kuwa serikali imedhamiria kupambana na rushwa?

https://p.dw.com/p/30jKy
Mandamano ya kupinga rushwa Kenya
Picha: Reuters/H. Kariuki

J2 0307 Kenya Corruption/First Governor to be prosecuted - MP3-Stereo

Mwanasheria mkuu wa Kenya Noordin Mohammed Haji amesema kuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa na tume ya kitaifa ya kupambana na ufisadi unaomhusisha Gavana wa Kaunti ya Busia, Sospeter Ojaamong na ufisadi wa kutumia vibaya ofisi yake pamoja na kula njama ya kutaka kuiba mamilioni ya fedha za umma. Ni mwanasiasa wa kwanza wa cheo cha gavana kuchukuliwa hatua hii katika kesi inayohusisha tuhuma za kutumia fedha nyingi katika miradi ya umma ambayo haijawahi kukamilishwa.

Je, ni kusema sasa serikali ya Kenya imedhamiria kweli kupambana na rushwa, na wanasemaje wachambuzi na wataalamu katika vita dhidi ya rushwa? Saumu Mwasimba amezungumza na mchambuzi na aliyewahi wakati mmoja  kuwa mkuu wa tume ya kitaifa ya kupambana na rushwa, Profesa Patrick Lumumba, na alikuwa na mtazamo huu.