Vettel: Ferrari itapambana vilivyo na Mercedes | Michezo | DW | 16.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Vettel: Ferrari itapambana vilivyo na Mercedes

Sebastian Vettel ambaye alimaliza katika nafasi ya tatu katika mbio za mkondo wa Australia katika timu yake mpya ya Ferrari, amesema kazi sasa ni kuhakikisha kuwa wanashindana vikali na Mercedes hadi mwisho.

Bingwa huyo mara nne wa ulimwengu alikuwa na furaha kuwa mmoja wa waliofika jukwaani kwa mara ya kwanza katika gari lake la Ferrari tangu alipoihama timu ya Red Bull.

Vettel sasa amesema anaangazia macho yake mashindano ya wikendi ijayo ya mkondo wa Malaysia. " tumekuwa na mashindano mazuri siyo tu katika kufuzu bali pia katika mashindano yenyewe na ni vizuri kujiunga nao na nnajivunia sana. Ipo kazi nyingi mbele yetu kujaribu kuwabwaga hawa wawili na kuipiku timu ya Mercedes na nina uhakika tutafaulu.

Lewis Hamiliton na Nico Rosberg walichukua nafasi ya kwanza na pili katika mashindano hayo ya jana ambayo ni ya kwanza msimu huu na kuhakikisha timu yao inaendelea kutawala Formula One baada ya kuwazidi nguvu wapinzani wao msimu uliopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com