1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Formula One

Mbio za magari zenye kasi zaidi na ghali zaidi duniani. Chimbuko hasa la Formula One ni barani Ulaya na hasa nchini Uingereza, ingawa Italia, Ujerumani na Ufaransa zilitoa mchango mkubwa katika kuundeleza mchezo huo.

Siku hizi karibu nusu ya mashindano ya msimu wa F1 yanafanyika katika mataifa mengine, yakitazamwa na hadhira ya karibu watu milioni 500 kila mwaka kupitia televisheni. Ujerumani ilisubiri kwa miongo kadhaa kabla ya kupata bingwa wake wa dunia wa mashindano ya F1, na kisha ikapata mabingwa wawili mfululizo. Michael Schumacher alishinda mataji saba ya madereva kati ya 1994 na 2004, Sebastian Vettel alishinda mataji manne mfululizo kati ya 2010 na 2013. Lewis Hamilton ndiyo bingwa wa sasa wa madereva, na timu yake ya Mercedes ikajinyakulia taji la ubora mwaka 2014. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui ya DW kuhusu mashindano ya Formula One.

Onesha makala zaidi