Verstappen aponyoka na ushindi wa Silverstone | Michezo | DW | 10.08.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Verstappen aponyoka na ushindi wa Silverstone

Dereva wa Red Bull Max Verstappen alionyesha umahiri wale na kushinda mbio za awamu ya 70 za Grand Prix katika uwanja wa Silverstone. Ushindi wake wa kwanza msimu huu uliotaliwa na Mercedes

Verstappen alianza mbio hizo katika nafasi ya nne na kuapa ushindi wa kwanza wa msimu, ambao umetawaliwa na Mercedes. Charles Leclerc wa timu ya Ferrari alimaliza katika nafasi ya nne baada ya kuanza mbio hizo katika nafasi ya nane, wakati dereva mwenza Mjerumani Sebastian Vettel akimaliza katika nafasi ya 12. "Ndiyo, gari letu lilikuwa na kasi sana. Sikuwa na matatizo yoyote ya matairi. Tuliendelea tu kupambana na mwishowe tukawa na matokeo mazuri ya ushindi na tukawa na siku nzuri. Tulikuwa na mkakati mzuri, kila kitu kilikwenda salama. Kwa hiyo nna furaha kushinda.

Bingwa mara sita wa ulimwengu Muingereza Hamilton anaendelea kuongoza msimamo wa ubingwa akiwa na pointi 107 huku Verstappen katika nafasi ya pili na 77 naye Bottas akikamata ya tatu na 73.