Vatican yajadili unyanyasaji wa kijinsia | Masuala ya Jamii | DW | 14.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Vatican yajadili unyanyasaji wa kijinsia

Katika muendelezo wa kampeni ya mageuzi yanayoongozwa na Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, mipango ya kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji itapewa kipaumbele na viongozi wote wa dini wa Kanisa Katoliki.

Papa Francis akiwa katika misa

Papa Francis akiwa katika misa

Mwanzoni kazi ya kamisheni hii ilipata pingamizi kubwa hasa pale hatua kali zilizoanzishwa na mtangulizi Papa Benedict wa 16 na kuendelezwa na Papa Francis dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia lakini sasa inakubalika kuwa ni njia nzuri itakayoleta mafanikio.

Papa Francis aliitangaza kamisheni hii mwaka 2013 kama jopo litalohusika kutoa elimu kwa kanisa juu ya njia zitakazofuatwa katika kuwalinda watoto na kuwang'oa wale wanaowadhalilisha kanisani.

Wanachama wa kamisheni hiyo wamepongeza hatua hiyo wakisema ni hatua kubwa iliyofikiwa hasa kutokana na lawama ambazo makasisi walikuwa wakibebeshwa kuhusiana na kuficha ukweli juu ya wachungaji waliokuwa wakiwanyanyasa watoto na hasa pale ilipojulikana kuwa wamehamishwa kutoka kwenye parokia walizohudumia na kupelekwa kwenye parokia nyingine badala ya kuwaripoti polisi.

Vatikanstaat Heiligsprechung Mutter Teresa durch Papst Franziskus

Waumini wa kanisa Katoliki katika misa mjini Vatican

Kwa miongo mingi tu, Vatican ilifumba macho na kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wachungaji na makasisi waliokuwa na wanawalinda katika maovu haya.

Wanachama wa kongamano hili tayari wameshawahutubia wachungaji, wafuasi na wanafunzi wa chuo cha diplomasia cha Vatican. Marie Collins kutoka Ireland ambaye ni mmoja kati ya manusura wa unyanyasaji wa kijinsia na kasisi Charles Scicluna aliyekuwa zamani mwendesha mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia watalihutubia kongamano litakalohudhuriwa na makasisi wapya. Wanatarajia kuwafunza mbinu za kuziendesha dayosisi zao.

Kongamano hili linafanyika mwaka mmoja baada ya Vatican kupata fedheha pale kasisi mmojaMmfaransa alipowambia makasisi kuwa haoni haja ya kuwaripoti kwa polisi wachungaji walioshukiwa kuhusika na makosa ya kuwabaka au kuwanyanyasa watoto. Padri huyo aliendelea kusema kwa mtazamo wake anafikiri jukumu hilo ni la wahanga au wazazi wa watoto waliofanyiwa vitendo hivyo, lakini hapo hapo Kadinali Sean O'Malley haraka akamrekebisha kwa kusema wachungaji na makasisi wana wajibu wa "maadili na mafundisho" unaowalazimu kuripoti makosa ya aina hiyo.

Miongoni mwa makasisi wanaotarajiwa kuhudhuria kongamano hilo wanatoka Afrika na bara Asia ambako mara nyingi viongozi wa makanisa wamekuwa wakikanusha kuwa vitendo vya unyanyasaji ni tatizo kubwa katika maeneo yao.

Upi ujumbe muhimu?

Kasisi Hans Zollner amesema ujumbe muhimu anaotaka kuutoa kwa makasisi wapya ni kwamba namnukuu "jambo la muhimu ambalo unaweza kufanya ni kama kasisi katika swala hili ni kuwasikiliza watu walionusurika, kwa kukaa nao na kuwapa muda wako na vile vile kuwasikiliza kwa moyo wako wote, yaani waonyeshe kuwa unawakaribisha kuwa nawe" mwisho wa kunukuu.

Papa Francis amepokea maombi ya kuacha utumishi kutoka kwa baadhi ya makasisi ingawa haijajulikana bado kama maombi haya ni kutokana na umri au ni kutokana na matatizo mengine yaliyowafanya makasisi hawa kuomba kung'atuka.

Mwandishi: Zainab Aziz/AP
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com