VARVASAINA:Moto unasambaa upya Ugiriki | Habari za Ulimwengu | DW | 26.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VARVASAINA:Moto unasambaa upya Ugiriki

Moto unaripotiwa kusambaa upya kwenye misitu na kuteketeza vijiji kadhaa katika eneo la kale la Olympia baada ya pepo kushika kasi.Takriban watu 51 wamethibitishwa kupoteza maisha yao na wengine wengi kuhofiwa kupotea katika mkasa wa moto ulio mbaya zaidi kutokea nchini humo katika kipindi cha muongo mmoja.

Eneo la magharibi la Peloponnese limeathirika zaidi huku wazima moto wakipambana kuokoa vijiji vilivyo karibu na eneo la kale la Olympia.Kengele za makanisa zilisikia katika kijiji kilicho karibu cha Kolyri wakati wakazi walikusanya virago vyao na kutoroka.

Ndege 6 za kuzima moto zilinyunyiza maji kwenye eneo hilo.Moto huo ulisambaa hadi kijiji cha karibu cha Varvasaina na kuteketeza nyumba kadhaa.Watu wanane wanaripotiwa kupoteza maisha yao katika eneo la mji wa Megalopolis kulingana na idara ya kuzima moto.Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya milimani ya Peloponnese na kisiwa cha Evia kilicho kaskazini mwa mji wa Athens.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com