1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama waimarishwa kisiwani Sri Lanka

4 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1rZ

COLOMBO:

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Sri Lanka Colombo,kisiwa hicho kikiadhimisha mwaka wa sitini tangu kupata uhuru wake.Siku ya Jumapili mshambulizi aliejitolea maisha muhanga alijiripua katika kituo cha treni mjini Colombo.Watu 29 waliuawa na zaidi ya 90 wengine wamejeruhiwa.Serikali imewalaumu waasi wa Tamil Tigers.Mapigano kati ya vikosi vya serikali na Tamil Tigers yameshika kasi baada ya serikali mwezi uliopita kujitoa kwenye makubaliano ya amani yaliotiwa saini miaka sita iliyopita.