1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa

11 Aprili 2026

Urusi na Ukraine leo zimebadilisha wafungwa 175 wa vita kwa kila upande kabla ya kuanza kwa mpango wa kusitisha mapigano kusherehekea Pasaka ya Kiorthodoksi.

https://p.dw.com/p/5C1mm
Marekani  Washington D.C. 2025 | Putin na Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia)Picha: Mandel Ngan/Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amethibitisha kuhusu hatua ya kubadilishana kwa wafungwa hao kupitia chapisho kwenye mtandao wa Telegram.

Zelensky amesema wanajeshi wao waliilinda Ukraine katika mistari ya mbele ya vita huko Mariupol, kwenye kinu cha nyuklia cha Chernobyl, katika mikoa ya Donetsk, Luhansk, Kharkiv, Kherson, Zaporizhzhya, Sumy, Kiev na Kursk.

Ameongeza kuwa baadhi yao walijeruhiwa na wengi wamekuwa kizuizini tangu mwaka 2022 lakini hatimaye wamerudi nyumbani.

Mara kwa mara, pande hizo mbili zimebadilishana wafungwa pamoja na miili ya wanajeshi waliouawa wakati wa vita hivyo ambavyo vimedumu sasa kwa zaidi ya miaka minne.