1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama UN kupigia kura azimio juu Gaza Jumatatu

Hawa Bihoga
23 Machi 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa limesogeza mbele tarehe ya kuipigia kura rasimu ya azimio la usitishwaji mara moja wa vita kati ya Israel na Hamas hadi siku ya Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4e3Mh
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifaPicha: Seth Wenig/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa fursa ya majadiliano zaidi. Awali rasimu hiyo ilikusudiwa kupigiwa kura leo Jumamosi.

Rasimu hiyo mpya inataka usitishwaji wa mara moja wa mapigano katika mwezi mtukufu unaoendelea wa Ramadhan na kisha baadaye yapatikane makubaliano ya kusitisha kabisa mapigano.

Wanachama wanane kati ya 10 wasio wa kudumu wa baraza hilo wamekuwa wakifanyia kazi rasimu hiyo, ambayo pia inataka kuachiliwa huru "mara moja na bila masharti" mateka wote waliochukuliwa na Hamas pamoja na kuondolewa kwa "vizuizi vyote" kwa misaada ya kibinadamu kuingia kwenye Ukanda wa Gaza.

Soma pia:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kupitisha azimio la kusitisha mapigano Gaza

Rasimu hiyo mpya inafuatia kushindwa kwa azimio lililopendekezwa na Marekani hapo jana Ijumaa. Urusi na China zilitumia kura za turufu kulipinga azimio hilo ambalo pia lilikataliwa na mataifa ya Kiarabu.