1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani vurugu za Israel katika Ukingo wa Magharibi

4 Juni 2024

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa wito hivi leo wa kukomesha ghasia zinazoendeshwa na vikosi vya usalama vya Israel na walowezi wa kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

https://p.dw.com/p/4gdog
Tingatinga la Israel likiwa kwenye mitaa ya mji wa Jewakati wa shambulio katika mji wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi.
Tingatinga la Israel likiwa kwenye mitaa ya mji wa Jewakati wa shambulio katika mji wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi.Picha: Zain Jaafar/AFP

Vurugu hizo zimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 500 tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas huko Gaza mnamo Oktoba 7 mwaka jana.

Soma pia:Qatar yataka misimamo ya wazi kuhusu mpango wa Gaza

Hayo yakijiri, Qatar ambayo ni mpatanishi katika mzozo huo imesema inasubiri "msimamo ulio wazi" kutoka  Israel kufuatia pendekezo la rais wa Marekani Joe Biden la kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka, pendekezo ambalo linamuweka matatani Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.