1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Watu 576,000 ukingoni mwa kutumbukia kwenye baa la njaa Gaza

28 Februari 2024

Maafisa wa ngazi ya juu katika mashirika ya Umoja wa Mataifa wametahadharisha kuwa takriban watu 576,000 katika ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye baa la njaa.

https://p.dw.com/p/4cxiP
Watoto wa Kipalestina wanashikilia sufuria tupu ili kugawiwa chakula kinachosambazwa na mashirika ya kutoa misaada
Watoto wa Kipalestina wanashikilia sufuria tupu ili kugawiwa chakula kinachosambazwa na mashirika ya kutoa misaadaPicha: Abed Zagout/Anadolu/picture alliance

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Ramesh Rajasingham amesema mtoto mmoja kati ya sita walio chini ya umri wa miaka miwili kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, anakabiliwa na utapiamlo.

Mkuu huyo ameongeza kuwa, watu wote milioni 2.3 katika ukanda huo wa Gaza wanategemea misaada ya chakula ili kuendelea kuishi.

Soma pia:  Israel yatishia kushambulia Rafah wakati wa Ramadhan

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Carl Skau ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, shirika hilo liko tayari kupeleka misaada ya kibinadamu kwa wahitaji huko Gaza iwapo kutakuwepo na makubaliano ya kusitisha mapigano.