1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Raia 33,000 wa Haiti wakimbia machafuko katika mji mkuu

22 Machi 2024

Zaidi ya watu 33,000 wamekimbia mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince mwezi huu wakati mji huo ulipotekwa na magenge yenye silaha na kusababisha machafuko ya kisiasa katika taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4e27H
 Haiti
Raia wa Haiti wakikimbia mapiganoPicha: Fran Afonso/REUTERS

Zaidi ya watu 33,000 wamekimbia mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince mwezi huu wakati mji huo ulipotekwa na magenge yenye silaha na kusababisha machafuko ya kisiasa katika taifa hilo .

Taarifa iliyotolewa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, imesema kuwa mashambulizi ya magenge na ukosefu wa usalama kwa ujumla, vinachangia watu zaidi kukimbia mji huo kutafuta hifadhi katika mikoa mingine na kuhatarisha maisha yao kwa kupita katika njia zinazodhibitiwa na magenge.Mazungumzo ya kuunda serikali yashika kasi nchini Haiti

IOM imesema kutoka Machi 8 hadi 20, waangalizi walihesabu kuondoka kwa watu 33,333 kutoka mji huo na kwamba inapaswa kusisitizwa kuwa mikoa hiyo haina miundo mbinu mwafaka na jamii za maeneo hayo pia hazina raslimali za kutosha kuziwezesha kushughulikia idadi hiyo kubwa ya watu wanaotafuta hifadhi.

Kulingana na Kundi linalofuatilia Migogoro ya Kimataifa, juhudi za kutafuta maelewano ya kisiasa zinakabiliwa na changamoto kubwa kwasababu magenge hayo tayari yameashiria kwamba hayatatambua serikali ya mseto ambayo inatarajiwa kuundwa katika siku zijazo.