1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wajadili chuki dhidi ya Waislamu

11 Julai 2023

Umoja wa Mataifa umesema kauli za chuki zimeenea kila mahali huku baraza lake la haki za binaadamu likijadili leo juu ya matukio ya hivi karibuni ya uchomaji wa kitabu kitukufu kwa Waislamu cha Qur'an.

https://p.dw.com/p/4Tjzo
Protest against the Quran Burning In London, UK - 28 Jan 2023
Picha: Loredana Sangiuliano/SOPA/ZUMA/picture alliance

Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema matukio hayo yamefanywa kimakusudi ili kuchochea hasira na kuzigawanya jamii.

Ameongeza kuwa watu wanahitaji kuheshimu imani na tamaduni za wengine licha ya kuwa na misimamo tofauti.

Soma zaidi: Erdogan aonya Sweden kuhusu NATO baada ya kuchomwa Quran

Nakala ya kitabu cha Qur'an ilichomwa mbele ya msikiti katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm, mnamo Juni 28 na kuibua ukosoaji mkubwa kutoka mataifa ya Kiislamu.

Pakistan na mataifa mengine yamehimiza kufanyika majadiliano juu ya matukio yaliyopangwa ya chuki dhidi ya Uislamu katika baadhi ya mataifa ya Ulaya.