1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umati wahudhuria maandamano HongKong licha ya mvua kali

Oumilkheir Hamidou
18 Agosti 2019

Maelfu ya wakaazi wa Hong Kong wamekusanyika katika bustani ya Victoria Park, na kuwabainishia maafisa wa serikali jinsi wanavyoungwa mkono na wananchi na wanaweza kuandamana kwa amani

https://p.dw.com/p/3O5EE
Hongkong Victoria Park Demonstration und Proteste
Picha: AFP/I. Lawrence

Wakazi wazee na familia wanajiunga na wanaharakati vijana na wengine wenye msimamo mkali katika maandamano hayo. Waandalizi wanakadiria watu wasiopungua milioni mbili wanashiriki katika maandamano hayo, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1997 katika maandamano jimboni humo. Polisi imeruhusu watu wakusanyike lakini wasiandamane.

Waandamanaji wameipuuza amri hiyo, wameteremka kwa wingi majiani kati kati ya Hong Kong licha ya mvuwa kali. "Ikiwa mbinu za Beijing na Hong Kong ni kuona vuguvugu letu linadhoofika, wamekosea...."hatutochoka." amesema Bonnie Leung wa shirika linalopigania haki za raia-CHRF.

Waandamanaji wamekamata bango lenye maandishi"Wahongo Kong hawatoachilia mbali madai yao
Waandamanaji wamekamata bango lenye maandishi"Wahongo Kong hawatoachilia mbali madai yaoPicha: picture-alliance/AP/Vincent Thian

Waandamanaji wamepania kutetea madai yao

Waandamanaji wanasema wamepania kuionyesha serikali hawatoachilia mbali madai yao matano ikiwa ni pamoja na kubatilisha mswaada wa sheria kuhusu kuhamishiwa China wahalifu na uchunguzi huru kuhusu matumizi ya nguvu ya polisi. Waandamanaji wanadai pia kiongozi wa serikali ya jimbo hilo Carrie Lam ajiuzulu.

 "Tutabakia hapa hapa, tutasimama kidete hadi wanatujibu. Kwa pamoja tuna nguvu zaidi," anasema mwanafunzi Harles Ho. Kijana huyo wa miaka 20 anasema mvua kali haitobadilisha msimamo wao.

Maandamano ya mjini Berlin kuwaunga mkono wafuasi wa serikali ya China
Maandamano ya mjini Berlin kuwaunga mkono wafuasi wa serikali ya ChinaPicha: picture-alliance/NurPhoto/E. Contini

Maandamano yamelengwa kuwa ya amani

Katika wakati ambapo matumizi ya nguvu yaligubika maandamano yao mnamo wiki za hivi karibuni, waandalizi wa maandamano ya leo wanawataraji kudhihiirisha "wakaazi wa Hong Kong wanaweza kuandamana kwa amani.

Waandamanaji shupavu walikosolewa wiki hii baada ya maandamano katika uwanja wa ndege wa kimataifa kumalizikia kwa mapigano dhidi ya  polisi wa kuzuwia fujo. Waandamanaji hao waliwazuwia abiria wasisafiri na baadae kuwavamia watu wawili waliokuwa wakiwatuhumu kuwa majasusi wa serikali uu ya China.

Picha hizo ziliifuja hadhi ya waandamanaji na kupelekea baadhi ya waandalizi kuomba radhi.

Vuguvugu la maandamano limeanza juni 9 iliyopita katika jimbo hilo la HongKong lililokuwa zamani likisimamiwa na Uingereza.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/dpa//AP

Mhariri: Buwayhid, Yusra