1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa kulinda amani utasalia Mali

30 Juni 2022

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura jana Jumatano kudumisha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali.

https://p.dw.com/p/4DTwk
Mali Armee Frankreich Ménaka Sahelzone
Picha: EtatMajordes Armées

Mali iliyokumbwa na machafuko, wakati wakilaani utawala wa kijeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi kwa kutumia mamluki wanaokuka haki za binadamu.

Baraza la usalama pia limeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuyumba kwa hali ya kisiasa na kudorora kwa hali ya usalama nchini Mali. Urusi na China hazikulipigia kura azimio hilo lililoandaliwa na Ufaransa ambalo linarefusha mamlaka ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali hadi Juni 30, mwaka ujao, na kiwango cha sasa cha maafisa 13,289 wa jeshi na  1,920 wa polisi ya kimataifa.

Kufuatia kura ya jana Jumatatno balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Nicolas De Riviere, amesema ukiukwaji wa haki za biandamu na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu kunakofanywa na makundi ya kigaidi pamoja na vikosi vya Mali pamoja na wanachama wa kampuni ya Wagner, lazima vikome.

Balozi huyo ametahadharisha kuhusu ongezeko la kudorora kwa hali ya usalama akisema ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchiniMali lazima uruhusiwa kuyafikia maeneo ambako matukio ya ukiukaji yanadaiwa kufanywa kukamilisha majukumu yake kwa mujibu wa mamlaka uliyo nayo. Ametaka kuchapishwe ripoti kila baada ya miezi minne kuhusu hali ya haki za binadamu kulingana na jinsi azimio hilo linavyoanisha. De Riviere ameongeza kusema wale wenye dhamana ya vitendo vya ukiukaji wa haki shari wawajibishwe na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Kutokana na msuguano na watawala wa kijeshiw a Mali, Ufaransa ilitangaza mnamo mwezi Februari mwaka huu wkamba vikosi vyake vingeondoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi kufikia msimu huu wa kiangazi. Lakini Ufanrasa ilipendekeza kuendelea kutoa msaada wa usalama wa anga kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Maifa, wanaohitaji uwezo wa helikopta za kufanyia mashambulizi. Hata hivyo Mali inapinga vikali uwezpo wa jeshi la anga la Ufaransa na pendekezo la Ufaransa lilitolewa kutoka kwenye azimio hilo na kutupwa kapuni.

Marekani yaliunga mkono azimio

Mali Symbolbild UN
Makao makuu ya MINUSMA, BamakoPicha: Nicolas Remene/Le Pictorium/imago images

Naibu balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Richards Mills amesema sababu moja kwa nini Marekani imeliunga mkono azimio hilo ni kwamba inalaani vikali ongezeko kubwa la kutisha la vitendo vya kukanyagwa kwa haki na udhalilishaji dhidi ya raia na kutoa wito tena kwa pande zote husika ziwache kuzikaba koo haki za binadamu au kufanya vitendo vya unyanyasaji. Mills aidha amesema hii inajumuisha makundi ya kigaidi, majeshi ya Mali na maafisa wa kampuni inayotoa huduma za usalama ya Wagner inayoungwa mkono na utawala wa Urusi, Kremlin.

Azimio hilo linaidhinisha tume ya Umoja wa Mataifa iwasaidie maafisa wa Mali katika kuimarisha na kuzilinda haki za binadamu. Kiksoi ha tume hiyo pia kinatakiwa kufuatilia, kuorodhesha, kufanya uchunguzi wa kutafuta taarifa, kusaidia uchunguzi na kuripoti hadharani mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na vitendo vya udhalilishaji wa utu wa watu wa Mali, ikiwemo unyanyasaji kingono na usafirishaji binadamu, na kutoa mchango katika juhudi za kuepusha vitendo vya ukiukaji na unyanyasaji.

Azimio hilo pia linaidhinisha walinda amani wa Umoja wa Mataifa wafanye majukumu mengine, yakiwemo kusaidia kutekeleza mkataba wa amani uliosainiwa mnamo Nuni 2015 na mchakato wa sasa wa kipindi cha mpito wa kisiasa., kusaidia kurejesha uthabiti wa dola katikati mwa Mali na kuimarisha usalama na ulinzi katika eneo hilo, huku wakiwalinda raia na kuweka mazingira salama kwa ajili ya kupelekwa misaada ya kiutu.

Urusi yalipinga azimio

Militär I Mali I UN-Truppr EUTM
Jeshi la MaliPicha: Nicolas Remene/Le Pictorium/MAXPPP/dpa/picture alliance

Akielezea hatua ya Urusi kutolipigia kura azimio hilo, naibu balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Anna Evstigneeva, amedokeza juu ya maneno yaliyotumiwa kuzungumzia haki za binadamu, akisema hayatasaidia kuhakikisha Mali inakuwa na uwezo wa kutumia haki yake ya kujilinda yenyewe pamoja na raia wake.

Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Mali linatoa uungwaji mkono wa baraza la usalama la umoja huo kwa kuendelea kutolewa msaada wa kikosi kinachopambana dhidi ya ugaidi kinachojulikana kama G5 Sahel, ambacho watawala wa kijeshi wa Mali wametangaza wanajitoa mnamo Mei mwaka huu.

Baraza la usalama limesema litaendelea kutoa huduma za matibabu na kuwahamisha majeruhi na pia mashine za kusaidia majeshu kupumua pamoja na matumizi ya kiwanda cha kutengeneza vifaa. Limemtaka katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuimarisha mabadilishano ya taarifa kati ya kikosi cha kulinda amani nchini Mali na mataifa ya kundi la G5 Sahel kwa kutoa taarifa muhimu zinazohitajika za kijasusi.

/AP